Taarifa hii ya faragha inatumika kwa tovuti, huduma na bidhaa za Microsoft ambazo hukusanya data na huonyesha masharti haya, na hata pia huduma zao za auni ya bidhaa. Haitumiki kwa tovuti, huduma na bidhaa za Microsoft ambazo hazionyeshi au kuunganishwa kwenye taarifa hii au ambazo zina taarifa zake za faragha.
Tafadhali soma muhtasari hapa chini na ubofye "Jifunze Mengi" kwa maelezo zaidi juu ya mada maalum. Huenda pia uteue kutoka kwa bidhaa zilizoorodheshwa hapa juu ili uone taarifa hiyo faragha ya bidhaa. Baadhi ya bidhaa, huduma au vipengele vilivyotajwa katika taarifa hii huenda visipatikane katika masoko yote. Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya ahadi ya Microsoft ili kulinda faragha yako katika http://www.microsoft.com/privacy.
Tovuti nyingi za Microsoft hutumia "vidakuzi", faili ndogo za matini ambazo zinaweza kusomwa na seva ya wavuti katika kikoa ambacho huweka kidakuzi. Huenda tukatumia vidakuzi ili kuhifadhi mapendeleo na mipangilio yako; msaada wa kuingia; kutoa matangazo yaliyolengwa; na kuchanganua shughuli za tovuti.
Sisi pia hutumia minara ya wavuti ili kusaidia kuwasilisha vidakuzi na kukusanya uchanganuzi. Huenda hii ikajumuisha minara ya wavuti ya wahusika wengine, ambao wamekatazwa dihid kukusanya maelezo yako ya kibinafsi.
Una zana kadhaa za kudhibiti vidakuzi na teknolojia sawa, ikiwa ni pamoja na:
Matumizi yetu ya Vidakuzi
Tovuti nyingi za Microsoft hutumia “vidakuzi,” ambavyo ni faili ndogo za matini zilizowekwa kwenye diski yako kuu na seva ya Wavuti. Vidakuzi vina matini ambayo yanaweza kusomwa na seva katika kikoa kilichotoa kidakuzi kwako. Matini hayo mara kwa mara huwa na utungo wa namba na herufi ambayo hutambua kipekee kompyuta yako, lakina huenda ikawa na maelezo mengine pia. Hapa kuna mfano wa matini yaliyohifadhiwa kwenye kidakuzi ambacho Microsoft huenda ikaweka kwenye diski kuu yako wakati unapotembelea moja ya tovuti zetu: E3732CA7E319442F97EA48A170C99801
Tunaweza tumia vidakuzi kwa:
Baadhi ya vidakuzi tunavyotumia sana vimeorodheshwa katika jedwali lifuatalo. Orodha hii sio kamili, lakini imekusudiwa kuonyesha baadhi ya sababu tunaweka vidakuzi. Kama utatembelea tovuti yetu, itaseti baadhi au vidakuzi vyote vifuatavyo:
Kwa kuongezea vidakuzi Microsoft huenda ikaweka wakati unapotembelea tovuti zetu, huenda wahusika wengine wakaweka pia vidakuzi vingine kwenye kiendeshi chako kikuu wakati unapotembelea tovuti za Microsoft. Katika visa vingine, hiyo ni kwa sababu tumeajiri wahusika wengine ili kutoa huduma zingine kwa niamba yako, kama vile uchanganuzi wa tovuti. Katika visa vingine, ni kwa sababu kurasa zetu za wavuti zina maudhui au matangazo kutoka kwa wahusika wengine, kama vile video, maudhui ya habari au matangazo yanayowasilishwa na mitandao mingine ya matangazo. Kwa sababu kivinjari chako kinaunganishwa kwenye seva hizo za wavuti za wahusika wengine ili kuepua maudhui hayo, wahusika hao wengine wanaweza kuweka au kusoma vidakuzi vyao wenyewe kwenye kiendeshi chao kikuu.
Jinsi ya Kudhibiti Vidakuzi
Kwa mfano, katika Internet Explorer 9, huenda ukafuta vidakuzi kwa kuchukua hatua zinazofuata:
Maagizo ya kuzuia vidakuzi kwenye vivinjari vingine viko kwenye http://www.allaboutcookies.org/manage-cookies/.
Tafadhali tambua kuwa kama utachagua kuzuia vidakuzi, huenda usiingie au hutumie vibambo tangamanishi vya tovuti za Microsoft na huduma ambazo hutegemea vidakuzi, na mapendeleo mengine yanayotegemea vidakuzi hayataweza kuheshimiwa.
Tafadhali tambua kuwa kama utachagua kufuta vidakuzi, kuseti kokote na mapendeleo yanayodhibitiwa na vidakuzi hivyo, kujumuisha na mapendeleo ya matangazo, zitafutwa na zitahitaji kuundwa tena.
Kivinjari dhibiti "Usifutilizie" na Ulinzi wa Ufuatilizi. Baadhi vivinjari vipya imejumuisha kipengele cha "Usifuatilizie". Vingi vya vipengele hivi, vinapowashwa, kutuma viashiria au pendeleo kwenye tovuti unatembelea ikiashiria kuwa hutaki kufuatiliziwa. Tovuti hizo (au maudhui ya nafsi ya tatu kwenye tovuti hizo) zinaweza kuendelea kujikita katika shughuli unaweza ukaona kama ufuatilizi hata kama umeazimia pendeleo, kulingana na usiri wa sera za tovuti hizo.
Internet Explorer 9 na 10 ina kipengele kinachoitwa Ulinzi wa Ufuatiliaji ambacho husaidia kuzuia tovuti unazotembelea dhidi ya kutuma kiotomatiki maelezo kuhusu ziara yako kwa watoa huduma wa maudhui ya wahusika wengine. Wakati unapoongeza Orodha ya Ulinzi wa Ufuatiliaji, Internet Explorer itazuia maudhui ya wahuka wengine, ikiwa ni pamoja na, kutoka kwa tovuti yoyote ambayo imeorodheshwa kama tovuti ya kuzuiwa. Kwa kuzuilia utembeleaji kwenye tovuti hizi Internet Explorer itazuilia taarifa ambazo tovuti hizi za nafsi ya tatu zinaweza kukusanya juu yako. Na wakati una Orodha ya Ulinzi wa Ufuatiliaji iliyowezeshwa, Internet Explorer itatuma mawimbi au mapendeleo ya Usifuatilie kwenye tovuti unazotembelea. Kwa kuongeza, katika Internet Explorer 10 unaweza ukaweka DNT "zimwa" au "washwa"ikijisimamia iwapo utapenda. Kwa maelezo zaidi kuhusu Orodha za Ulinzi wa Ufuatiliaji na Usifuatilizie, tafadhali angalia Taarifa ya faragha ya Internet Explorer au Msaada wa Internet Explorer.
Makampuni ya utangazaji huenda pia yakatoa uwezo wao mwenyewe wa kuchagua-kutoka pamoja na chaguo zaidi mahiri za utangazaji. Kwa mfano, mapendeleo ya utangazaji ya Microsoft na vidhibiti vya kuchagua-kutoka yanapatikana katika http://choice.live.com/advertisementchoice/. Tafadhali kumbuka kwamba kuchagua-kutoka hakumaanishi kwamba utakoma kupokea matangazo au kuona matangazo machache; hata hivyo, ukichagua kutoka, matangazo unayopokea hayatakuwa matangazo lengwa ya tabia. Na ziada, kujitoa hakusitishi taarifa kuingia kwenye seva zetu, lakini inasitisha uundaji wetu au usasishaji wa maumbo ambayo huenda yanatumiwa kwenye matangazo ya mienendo.
Matumizi yetu ya Web Beacons
Kurasa tovuti za Microsoft huenda zikawa na picha za kielektroniki zinazoitwa web beacons- wakati mwingine huitwa single-pixel gifs- huenda zikatumiwa kuwasilisha vidakuzi kwenye tovuti zetu, hebu na tuhesabu watumiaji ambao wametembelea kurasa hizo na kutoa huduma zilizonembwa kwa ushirika. Huenda tukajumuisha minara ya Wavuti katika ujumbe wa matangazo wa barua pepe au majarida yetu ili kubainisha kama ujumbe umefunguliwa na kushughulikiwa.
Tunaweza kufanya kazi na kampuni nyingine ambazo hutangaza katika tovuti za Microsoft ili kuweka beacons za tovuti kwenye tovuti zao au kwenye matangazo yao ili kutuwezesha kukuza takwimu kwamba ni vipi kubofya kawaida katika tangazo katika tovuti ya Microsoft inachangia kununua au hatua nyingine kwa tovuti ya mtumiaji.
Mwishowe, huenda tovuti za Microsoft zikawa na minara ya Wavuti kutoka kwa wahusika wengine ili kutusaidia kuchanganya takwimu zilizokusanywa zinazohusiana na ubora wa kampeni zetu za matangazo au shughuli zingine za tovuti zingine. Minara hii ya wavuti huenda ikaruhusu wahusika wengine kuweka au kusoma kidakuzi kwenye kompyuta yako. Tunawazuia wahusika wengine dhidi ya kutumia minara ya wavuti kwenye tovuti zetu ili kukusanya au kufikia maelezo yako ya kibinafsi. Hata hivyo, unaweza kuchagua kutoka kwa ukusanyaji data au kutumiwa na makampuni mengine ya uchanganuzi ya wahusika wengine kwa kubofya viungo vya kila moja vya watoa huduma wafuatao wa uchanganuzi:
Teknolojia Zingine Sawa
Kwa kuongezea vidakuzi vya kawaida na minara ya wavuti, tovuti zinaweza kutumia teknojia zingine ili kuhifadhi na kusoma faili za data kwenye kompyuta yako. Huenda hii ikafanyika ili kudumisha mapendeleo yako au kuboresha kasi na utendaji kazi kwa kuhifadhi faili zingine kindani. Lakini, kama vidakuzi vya kawaida, inaweza pia kutumiwa kuhifadhi kitambuaji cha kipekee cha kompyuta yako, ambacho kinaweza kutumiwa tena kufuatilia tabia. Teknolojia hizi hujumuisha Vipengee Gawize vya Ndani (au "Vidakuzi mweka") na Hifadhi ya Programu ya Silverlight.
Vipengee Gawize vya Ndani au "Vidakuzi mweka." Tovuti zinazotumia Teknolojia za Adobe Flash huenda zikatumia Vipengee Gawize vya Ndani au "Vidakuzi mweka" ili kuhifadhi data kwenye kompyuta yako. Kumbuka kwamba uwezo wa kufuta vidakuzi vya Mweka huenda vidhibitiwe au visidhibitiwe na mpangilio wa kivinjari chako kwa vidakuzi vya kawaida kwa kuwa hiyo huenda ikatofautiana na kivinjari. Ili kudhibiti au kuzuia vidakuzi vya Mweka, nenda kwa http://www.macromedia.com/support/documentation/en/flashplayer/help/settings_manager.html.
Hifadhi ya Programu ya Silverlight. Tovuti au programu ambazo hutumia teknolojia ya Microsoft Silverlight pia huwa na uwezo wa kuhifadhi data kwa kutumia Hifadhi ya Programu ya Silverlight. Kujifunza jinsi ya kudhibiti au kuzuia hifadhi kama hiyo, tembelea Silverlight.
Microsoft hukusanya aina nyingi ya maelezo ili kufanya kazi vizuri na kukupa bidhaa, huduma na uzoefu bora kama tuwezavyo.
Tunakusanya maelezo wakati unapojisajili, kuingia na kutumia tovuti na huduma zetu. Huenda pia tukapata maelezo kutoka kwa makampuni mengine.
Tunakusanya maelezo haya kwa njia mbalimbali, ikijumuisha kutoka kwa fomu za wavuti, teknolojia kama vile vikaduzi, kumbukumbu ya wavuti kwenye kompyuta yako au kifaa kingine.
Microsoft hukusanya aina nyingi ya maelezo ili kufanya kazi vizuri na kukupa bidhaa, huduma na uzoefu bora kama tuwezavyo. Baadhi ya maelezo haya unatupa moja kwa moja. Mengine tunayapata kwa kuzingatia jinsi unavyoingiliana na bidhaa na huduma zetu. Mengine yanapatikana kutoka kwa vyanzo vingine ambayo vinaweza kujumuisha data tunayokusanya moja kwa moja. Bila kujali chanzo, tunaamini ni muhimu kushughulikia maelezo hayo kwa makini na kusaidia kudumisha faragha yako.
Tunayokusanya:
Tunatumia mbinu kadhaa na teknolojia ili kukusanya maelezo kuhusu unavyotumia tovuti na huduma zetu, kama vile:
Microsoft hutumia maelezo tunayoyakusanya ili kutekeleza, kuboresha na kugeuza kukufaa bidhaa na huduma tunazozitoa.
Huenda pia tukatumia maelezo ili kuwasiliana na wewe, kwa mfano, kukufahamisha kuhusu akaunti yako na visasisho vya usalama.
Na huenda pia tukatumia maelezo ili kusaidia kutengeneza matangazo unayoona kwenye huduma zetu zinazoauniwa na matangazo muhimu zako.
Microsoft hutumia maelezo tunayoyakusanya ili kuendesha, kuboresha na kugeuza kukufaa bidhaa na huduma tunazotoa. Maelezo yaliyokusanywa kupitia huduma moja ya Microsoft huenda yakachanganywa na maelezo yaliyokusanywa kupitia huduma zingine za Microsoft ili kukupa uzoefu zaidi dhabiti na wa kibinafsi katika maingiliano yako na sisi. Huenda pia tukaongezea haya na maelezo kutoka kwa makampuni mengine. Kwa mfano, huenda tukatumia huduma kutoka makampuni mengine ili kutusaidia kupata eneo la jumla la jiografia juu ya anwani yako ya IP ili kugeuza baadhi ya huduma kufaa eneo lako la jiografia.
Huenda pia tukatumia maelezo ili kuwasiliana na wewe, kwa mfano, kukufahamisha wakati usajili unaisha, kukujulisha wakati visasisho vya usalama vinapatikana au kukujulisha wakati unahitaji kuchukua hatua ili kuweka akaunti yako ikitumika.
Microsoft hutoa nyingi kati ya tovuti na huduma zetu bure bila malipo kwa sababu zinaauniwa na utangazaji. Ili kufanya huduma hizi zipatikane sana, maelezo tunayoyakusanya huenda yakatumiwa ili kusaidia kuboresha matangazo unayoona kwa kuyafanya muhimu zaidi kwako.
Isipokuwa kama ilivyofafanuliwa katika taarifa ya hii ya faragha, hatutafichua maelezo yako ya kibinafsi kwa wahusika wengine bila kibali chako.
Tafadhali angalia Maelezo Mengine Muhimu ya Faragha kwa maelezo kuhusu wakati tunaweza kufichua maelezo, ikiwa ni pamoja na wabia na wachuuzi wa Microsoft, wakati inapohitajika na sheria au kuitikia mchakato wa kisheria, ili kukabiliana na ulaghai au kulinda maslahi yetu, au kulinda maisha.
Isipokuwa kama ilivyofafanuliwa katika taarifa hii ya faragha, hatutafichua maelezo yako ya kibinafsi kwa wahusika wengine bila kibali chako.
Bofya hapa kwa maelezo zaidi juu ya kushiriki au kufichua maelezo ya kibinafsi:
Baadhi ya huduma za Microsoft hukupa uwezo wa kuona au kuhariri maelezo yako ya kibinafsi mtandaoni.. Ili kusaidia kuwazuia wengine dhidi ya kuona maelezo yako ya kibinafsi, utahitajika kwanza kuingia. Jinsi unavyoweza kukufikia maelezo yako ya kibinafsi utategemea tovuti au huduma ulizotumia..
Microsoft.com - Unaweza kufikia na kusasisha maelezo yako mafupi kwenye Microsoft.com kwa kutembelea Kituo cha Maelezo Mafupi cha Microsoft.com.
Utozaji wa Microsoft na Huduma za Akaunti - Ikiwa una akaunti ya Utozaji ya Microsoft, unaweza kuongeza au kusasisha maelezo yako kwenye Tovuti ya Utozaji ya Microsoft kwa kubofya kwenye viungo vya “Maelezo ya Kibinafsi” au “Maelezo ya Utozaji".
Microsoft Connect - kiwa wewe ni mtumiaji aliyesajiliwa wa Microsoft Connect, unaweza kufikia na kuhariri maelezo yako ya kibinafsi kwa kubofya Dhibiti Maelezo yako Mafupi ya Connect kwenye tovuti ya Microsoft Connect.
Windows Live - Ikiwa umetumia huduma za Windows Live, unaweza kusasisha maelezo yako mafupi, kubadilisha nywila yako, kuona Kitambulishi cha kipekee kinachohusishwa na hati tambulishi zako. au kufunga akaunti zingine kwa kutembelea Huduma za Akauntiza Windows Live.
Maelezo Mafupi ya Umma ya Windows Live- Ikiwa umeunda maelezo mafupi ya umma kwenye Windows Live, huenda pia ukahariri au kufuta maelezo katika maelezo yako mafupi ya umma kwa kwenda kwenye Maelezo Mafupi ya Windows Live.
Utangazaji wa Kutafuta - Ikinunua utangazaji wa kutafuta kupitia Utangazaji wa Microsoft, unaweza kuhakiki na kuhariri maelezo yako ya kibinafsi kwenye Tovuti ya Microsoft adCenter.
Mipango ya Wenzi wa Microsoft - Ikiwa umejisajili na Mipango ya Wenzi wa Microsoft, unaweza kuhakiki na kuhariri maelezo yako mafupi kwa kubofya Dhibit Akaunti Yako kwenye Tovuti ya Mpango wa Wenzi.
Xbox - Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Xbox LIVE au Xbox.com, unaweza kuona au kuhariri maelezo yako ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na utozaji na maelezo ya akaunti, mipangilio ya faragha, usalama wa mtandaoni na mapendeleo ya kushiriki data kwa kufikia My Xbox kwenye kiweko cha Xbox 360 au kwenye tovuti ya Xbox.com. Kwa maelezo ya akaunti chagua My Xbox, Akaunti. Kwa mipangilio mingine ya maelezo ya kibinafsi, chagua My Xbox, kisha Maelezo mafupi, Mipanglio ya Usalama wa Mtandaoni.
Zune - Ikiwa una akaunti ya Zune au usajili wa Zune pass, unaweza kuona na kuhariri maelezo yako ya kibinafsi kwenye Zune.net net (ingia, fikia lebo yako ya Zune kisha Akaunti Yangu au kupitia programu ya Zune, (ingia, fikia lebo yako ya Zune, kisha chagua maelezo mafupi ya Zune.net.)"
Iwapo huwezi kufikia data ya kibinafsi iliyokusanywa kwa tovuti au huduma za Microsoft kupitia viungo hapa juu, huenda tovuti na huduma hizi zikakupa njia zingine za kufikia data yako. Unaweza kuwasiliana na Microsoft kwa kutumia fomu ya wavuti. Tutajibu maombi ya kufikia au kufuta maelezo yako ya kibinafsi kati ya siku 30.
Wakati tovuti au huduma ya Microsoft inapokusanya maelezo ya umri, itawazuia watumiaji chini ya umri wa miaka 13 au itapata kibali kutoka kwa mzazi au mlezi kabla ya mtoto wao kuitumia.
Wakati kibali kinapotolewa, akaunti ya mtoto hushughulikiwa kama akaunti yoyote ile, ikiwa ni pamoja na kuweza kuwasiliana na watumiaji wengine.
Wazazi wanaweza kubadilisha au kubatilisha kibali kama ilivyofafanuliwa katika taarifa hii ya faragha.
Wakati tovuti au huduma ya Microsoft inapokusanya maelezo ya umri, aidha iwatazuia watumiaji chini ya umri wa miaka 13 au itawauliza watoe kibali kutoka kwa mzazi au mlezi kabla waweza kuitumia. Hatutawauliza watoto chini ya umri wa miaka 13 kwa kujua watoe maelezo zaidi kuliko inavyofaa ili tutoe huduma.
Wakati kibali kimetolewa, akaunti ya mtoto inashughulikiwa kama akaunti yoyote ile. Huenda mtoto akaweza kufikia huduma za mawasiliano kama vile barua pepe, ujumbe wa papo hapo na bao za ujumbe mtandaoni na huenda wakaweza kuwasiliana huru na watumiaji wengine wa umri wowote..
Wazazi wanaweza kubadilisha au kubatilisha chaguo za kibali zilizofanywa awali, na kuhakiki, kuhariri au kuomba ufutaji wa maelezo ya kibinafsi ya watoto wao. Kwa mfano, kwenye Windows Live, wazazi wanaweza kutembelea Akaunti yao, na kubofya kwenye "Vibali vya Wazazi".
Matangazo mengi ya mtandaoni kwenye tovuti na huduma za Microsoft huonyeshwa na Utangazaji wa Microsoft. Wakati tunapokuonyesha matangazo ya mtandaoni, tutaweka kidakuzi kimoja au zaidi ili tutambue kompyuta yako kila wakati tunapokuonyesha tangazo. Baada ya muda, huenda tukakusanya maelezo kutoka kwa tovuti ambapo tunaweka matangazo na kutumia maelezo ili kusaidia kutoa matangazo zaidi muhimu.
Huenda ukasitisha kupokea matangazo yaliyolengwa kutoka kwa Utangazaji wa Microsoft kwa kutembelea ukurasa wetu wa toka.
Tovuti zetu nyingi na huduma za mtandaoni zinaauniwa na utangazaji.
Matangazo mengi ya mtandaoni kwenye tovuti na huduma za Microsoft huonyeshwa na Utangazaji wa Microsoft. Wakati tunapokuonyesha matangazo ya mtandaoni, tutaweka kidakuzi kimoja au zaidi kwenye kompyuta yako ili tutambue kompyuta yako kila wakati tunapokuonyesha tangazo. Kwa sababu tunawezesha matangazo kwenye tovuti zetu na hata pia kwa za wenzi wetu wa utangazaji na uchapishaji, tunaweza kuchanganya maelezo baada ya muda kuhusu aina za kurasa, maudhui na matangazo ambayo wewe, au wengine ambao wanatumia kompyuta yako, walitembelea au kuona. Maelezo haya hutumiwa kwa madhumuni mengi, kwa mfano, hutusaidia kuhakikisha kwamba hauoni matangazo yale yale tena na tena. Tunatumia tena maelezo haya ili kusaidia kuchagua na kuonyesha matangazo yaliyolengwa ambayo tunaamini huenda yakakuvutia.
Huenda ukasitisha kupokea matangazo yaliyolengwa kutoka kwa Utangazaji wa Microsoft kwa kutembelea ukurasa wetu wa toka. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi Utangazaji wa Microsoft hukusanya na kutumia maelezo, tafadhali angalia Taarifa ya Faragha ya Utangazaji wa Microsoft.
Tunaruhusu pia makampuni mengine ya matangazo, ikiwa ni pamoja na mitandao mingine ya matangazo, kuonyesha matangazo kwenye tovuti zetu. Katika kesi zingine, wahusika hawa watatu huenda wakaweka vidakuzi kwenye kompyuta yako. Makampuni haya kwa sasa ni pamoja na, lakini hayajuzuiliwa kwa: 24/7 Real Media, adblade, AdConion, AdFusion, Advertising.com, AppNexus, Bane Media, Brand.net, CasaleMedia, Collective Media, InMobi, Interclick, Jumptap, Millennial Media, Nugg.ad AG, Mobclix, Mojiva, SpecificMedia, Tribal Fusion, ValueClick, Where.com, Yahoo!, YuMe, Zumobi. Makampuni haya huenda yakakupa njia ya kutoka kwenye matangazo ya kulenga kulingana na vidakuzi vyao. Huenda ukapata maelezo zaidi kwa kubofya kwenye majina ya kampuni hapa juu na kwa kufuata viungo vya Tovuti za kila kampuni. Nyingi ya hizo pia ni wanachama wa Uvumbuzi wa Utangazaji wa Mtandao au Muungano wa Utangazaji wa Dijitali, ambayo kila moja hutoa njia rahisi ya kutoka kwenye matangazo ya kulenga kutoka kwa makampuni husika.
Unaweza kukomesha uwasilishaji wa barua pepe za matangazo za baadaye kutoka kwa tovuti na huduma za Microsoft kwa kufuata maagizo maalum katika barua pepe uliyopokea. Kulingana na huduma mahsusi, huenda pia ukawa na chaguo la kufanya chaguo amilifu kuhusu upokeaji wa barua pepe ya matangazo, simu, na barua ya posta ya tovuti au huduma mahsusi za Microsft.
Ukipokea barua pepe za matangazo kutoka kwetu na ungependa kukomesha kuzipata baadaye, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata maagizo katika ujumbe huo.
Kulingana na huduma mahsusi, huenda pia ukawa na chaguo la kufanya chaguo amilifu kuhusu upokeaji wa barua pepe ya matangazo, simu, na barua ya posta kutoka kwa tovuti au huduma mahsusi za Microsft kwa kutembelea na kuingia kwenye kurasa zinazofuata:
Chaguo hizi hazitumiki kwa uonyesho wa utangazaji wa mtandaoni: tafadhali rejelea sehemu ya “Uonyeshaji wa Utangazaji (Toka)" kwa maelezo juu ya suala hili. Wala hazitumiki kwa mpokeaji wa mawasiliano ya lazima ya huduma ambayo huzingatiwa sehemu ya huduma zingine za Microsoft, ambayo huenda ukapokea mara kwa mara isipokuwa ughairi huduma.
Wakati unapotumia huduma kutokana na mahali au kipengele , data ya seli ya jengo linalopatikana, data ya Wi-Fi na Mfumo Wa Mahali ulimwenguni (GPS) huenda ikatumwa kwa Microsoft Microsoft hutumia taarifa ya mahali ya ili kuweza kutoa huduma unazoomba, binafsisha hali yako ya matumizi na uboreshe bidhaa na huduma za Microsoft.
Huduma fulani huenda zikakuruhusu kudhibiti wakati ambapo taarifa ya mahali itatumwa kwa Microsoft au itapatikana na wengine. Katika hali fulani, katika baadhi ya hali taarifa ya mahali ni muhimu katika huduma na huenda ikahitaji, na huenda ukahitajika kusakinusha kipengele au kukatiza huduma hili kusitisha kutumwa kwa taarifa ya mahali. Rejelea uwekaji rekodi uliokuja na mtambo wako kwa taarifa kuhusu namna ya kuzima vipengele vya mahali.
Data ya Usaidizi ni maelezo tunayokusanya unapowasilisha ombi la usaidizi au kuendesha kitatuzi kiotomatiki, ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu maunzi, programu, na maelezo mengine yanayohusiana na tukio la usaidizi, kama vile: maelezo ya uthibitishaji au ya mwasiliani, ubinafsishaji kipindi cha gumzo, maelezo kuhusu hali ya mashine na programu kutoka wakati wa kutokea kwa shida na wakati wa uchunguzaji, data ya usajili na mfumo kuhusu usakinishaji wa programu na usanidi wa maunzi, na faili za kufuatilia hitilafu. Tunatumia Data ya Usaidizi kama ilivyoelezwa katika maelezo haya ya ya faragha, na kuongezea kuitumia kusuluhisha tukio lako la usaidizi na kwa madhumuni ya mafunzo.
Usaidizi unaweza kutolewa kwa njia ya simu, barua pepe, au gumzo la mtandaoni. Tunaweza kutumia Ufikiaji wa Mbali (RA), kwa kibali chako, kuenda kwenye eneo-kazi lako kwa muda. Mazungumzo ya simu, vipindi vya gumzo la mtandaoni, au vipindi vya Ufikiaji wa Mbali vikiwa na wataalam wa usaidizi vinaweza kurekodiwa na/au kufuatiliwa. Kwa RA, unaweza pia kufikia rekodi baada ya kipindi chako. Kwa Gumzo la Mtandaoni au RA, unaweza kukamilisha kipindi wakati wowote utakaochagua.
Kutokana na tukio la usaidizi, tunaweza kukutumia utafiti kuhusu matoleo na utumiaji wako. Lazima uchague kuondoka kwenye utafiti wa usaidizi kando na mawasiliano mengine yanayotolewa na Microsoft, kwa kuwasiliana na Usaidizi au kupitia kijachini cha barua pepe.
Ili kukagua na kuhariri maelezo yako binafsi yaliyokusanywa kupitia huduma zetu za usaidizi, tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia ya fomu ya Wavuti.
Wateja wengine wa biashara wanaweza kununua matoleo bora ya usadizi (mf. Kuu n.k.). Matoleo haya yanafidiwa na arifa na masharti yayo yenyewe.
Data ya Malipo ni taarifa unayotoa wakati unapofanya ununuzi mtandaoni. Hii inaweza kujumuisha nambari yako ya mtambo wa malipo (k.m., kadi ya mkopo, PayPal), jina lako na anwani ya anayelipia, na msimbo wa usalama unaohusiana na mtambo wako wa malipo (m.f., ile CSV au CVV). Sehemu hii inatoa taarifa ya ziada inayohusiana na mkusanyiko na matumizi ya taarifa yako ya malipo.
Data ya Malipo ni taarifa unayotoa wakati unapofanya ununuzi mtandaoni. Hii inaweza kujumuisha nambari yako ya mtambo wa malipo (k.m., kadi ya mkopo, PayPal), jina lako na anwani ya anayelipia, na msimbo wa usalama unaohusiana na mtambo wako wa malipo (k.m., ile CSV au CVV). Sehemu hii inatoa taarifa ya ziada inayohusiana na mkusanyiko na matumizi ya taarifa yako ya malipo.
Taarifa ya malipo unayotoa itatumiwa kukamilisha muamala wako, pia kwa ugunduzi na uzuizi wa udanganyifu. Kwa uhimili wa matumizi haya, huenda Microsoft ikashiriki taarifa na benki na mashirika mengine ambayo yanachakata miamala ya malipo, na kwa uzuiaji wa udanganyifu na upunguzfu wa hatari ya mkopo.
Unapotoa Data ya Malipo ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya Microsoft au mpangilio tutaweza kuhifadhi data hiyo ili ikusaidie kujaza katika siku zijazo.
Huenda unaweza kusasisha au kuondoa taarifa ya chombo cha malipo inayohusiana na akaunti yako ya Microsoft kwa kuingia kwenye https://commerce.microsoft.com. Huenda ukaondoa taarifa ya chombo chako cha malipo inayohusiana na akaunti ya shirika lako kwa kuwasiliana na Msaada kwa Mteja. Baada ya kufunga akaunti yako au kuondoa chombo cha malipo, hata hivyo, huenda Microsoft ikamiliki data ya chombo chako cha malipo kadri inavyohitajika ili kukamilisha muamala wako uliopo na kwa ugunduzi na uzuiaji wa udanganyifu.
Akaunti ya Microsoft (iliyojulikana awali kama Kitambulishi cha Windows Live na Microsoft Passport) ni huduma ambayo hukuwezesha kuingia kwenye bidhaa, tovuti na huduma za Microsoft, na hata pia zile za wabia walioteuliwa wa Microsoft. Wakati unaunda akaunti ya Microsoft, tutakuomba utoe maelezo mengine. Wakati unapoingia kwenye tovuti au huduma kwa kutumia akaunti yako ya Microsoft, tunakusanya maelezo mengine ili kuthibitisha kitambulisho chako kwa niaba ya tovuti au huduma, ili kukulinda dhidi ya akaunti mbaya, na kulinda ubora na usalama wa huduma ya akaunti ya Microsoft. Tunatuma pia maelezo mengine kwa tovuti au huduma uliyoingia na akaunti yako ya Microsoft.
Ili kuona maelezo ya ziada kuhusu akaunti ya Microsoft, ikiwa ni pamoja na kuunda na kutumia akaunti ya Microsoft, jinsi ya kuhariri maelezo ya akaunti, na jinsi tunavyokusanya na kutumia maelezo kuhusiana na akaunti ya Microsoft, tafadhali bofya Jifunze Zaidi.
Akaunti ya Microsoft (iliyojulikana awali kama Kitambulishi cha Windows Live na Microsoft Passport) ni huduma ambayo hukuruhusu kuingia kwenye bidhaa, tovuti na huduma za Microsoft, na hata pia zile za wabia walioteuliwa wa Microsoft. Hii hujumuisha bidhaa, tovuti na huduma kama zifuatazo:
Kuunda akaunti ya Microsoft.
Unaweza kuunda akaunti ya Microsoft hapa kwa kutoa anwani ya barua pepe, nywila na "dhibitisho zingine za akaunti", kama vile anwani mbadala ya barua pepe, namba ya simu, na swali na jibu la siri. Tutatumia "dhibitisho za akaunti" yako kwa malengo ya usalama tu - kwa mfano, kuthibitisha kitambulisho chako iwapo huwezi kufikia akaunti yako ya Microsoft na unahitaji msaada, au kuweka upya nywila ikiwa huwezi kufikia anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya Microsoft. Baadhi ya huduma huenda zikahitaji usalama uliongezwa, na katika kesi hizi, huenda ukaulizwa uunde ufunguo wa ziada wa usalama. Anwani ya barua pepe na nywila ambayo unatumia kujiandikisha kwa akaunti yako ya Microsoft ni "hati tambulishi" zako ambazo utatumia kuhalalisha na mtandao wetu. Zaidi,, namba ya kipekee ya Kitambulishi ya biti 64 itapangiwa hati tambulishi zako na itatumiwa ili kutambua hati tambulishi zako na maelezo husika.
Wakati unaunda akaunti ya Microsoft, tutauliza pia utoe maelezo yafuatayo ya kidemografia: jinsia; nchi; tarehe ya kuzaliwa; na msimbo wa posta. Huenda tukatumia tarehe ya kuzaliwa ili kuthibitisha kwamba watoto wamepata kibali kinachofaa kutoka kwa mzazi au mlezi ili kutumia akaunti ya Microsoft, kama inavyohitajika na sheria ya nchi. Kwa kuongezea, maelezo haya ya kidemografia hutumiwa na mifumo yetu ya utangazaji mtandaoni ili kukupa matangazo yaliyobinafsishwa kuhusu bidhaa na huduma zinazoweza kukusaidia, lakini mifumo yetu ya utangazaji haipati jina lako au maelezo ya mawasiliano. Kwa maneno mengine, mifumo yetu ya utangazaji haina au haitumii maelezo yoyote ambayo yanaweza kukutambua kibinafsi na moja kwa moja (kama vile jina lako, anwani ya barua pepe na namba ya simu). Kama unapendelea kutopokea matangazo yaliyobinafsishwa, unaweza kusajili mapendeleo yako na akaunti yako ya Microsoft kwa kutembelea ukurasa huu ili wakati wowote unapoingia kwenye tovuti au huduma na akaunti yako ya Microsoft, mifumo yetu ya utangazaji haitakupa matangazo yaliyobinafsishwa. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi Microsoft hutumia maelezo kwa ajili ya utangazaji, tafadhali angalia Nakala ya Nyongeza ya Faragha ya Utangazaji wa Microsoft.
Unaweza kutumia anwani ya barua pepe iliyotolewa na Microsoft (kama vile zile zinazoisha na live.com, hotmail.com, au msn.com) au anwani ya barua pepe inayotolewa na wahusika wengine (kama vile zinazoisha na gmail.com au yahoo.com) wakati unapojiandikisha kupata akaunti yako ya Microsoft.
Baada ya kuunda akaunti ya Microsoft, tutakutumia barua pepe inayokuuliza uthibitishe kwamba wewe ni mmiliki wa anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya Microsoft. Hii imeundwa ili kuthibitisha uhalali wa anwani ya barua pepe na kusaidia kuzuia anwani za barua pepe dhidi ya kutumiwa bila idhini ya wamiliki. Baada ya hiyo, tutatumia anwani hiyo ya barua pepe kutuma mawasiliano yanayohusiana na matumizi yako ya bidhaa na huduma za Microsoft; huenda pia tukakutumia barua pepe za matangazo kuhusu bidhaa na huduma za Microsoft kama inavyoruhusiwa na sheria za nchi. Kwa maelezo kuhusu kudhibiti mawasiliano yako ya matangazo, tafadhali tembelea Mawasiliano.
Ukijaribu kusajili akaunti ya Microsoft na upate kwamba mtu mwingine ameunda tayari hati tambulishi na anwani yako ya barua pepe kama jina la mtumiaji, unaweza kuwasiliana na sisi na uombe kwamba mtu yule mwingine achukue jina tofauti la mtumiaji ili uweze kutumia anwani yako ya barua pepe wakati unaunda hati tambulishi zako.
Kuingia kwenye programu, tovuti au huduma na akaunti yako ya Microsoft.
Wakati unapoingia kwenye tovuti au huduma kwa kutumia akaunti yako ya Microsoft, tunakusanya maelezo mengine ili kuthibitisha kitambulisho chako kwa niaba ya tovuti au huduma, ili kukulinda dhidi ya akaunti mbaya, na kulinda ubora na usalama wa huduma ya akaunti ya Microsoft. Kwa mfano, wakati unapoingia, huduma ya akaunti ya Microsoft hupokea na kuhifadhi hati tambulishi zako na maelezo mengine, kama vile namba ya kitambulishi ya kipekee ya biti 64 iliyopangiwa hati tambulishi zako, anwani yako ya IP, toleo lako la kivinjari cha wavuti, na muda na saa. Zaidi, kama unatumia akaunti ya Microsoft kuingia kwenye kifaa au kwenye programu ambayo imesakinishwa kwenye kifaa, kitambulishi cha kipekee kisichokuwa na mpangilio hupangiwa kifaa; kitambulishi hiki cha kipekee kisichokuwa na mpangilio kitatumwa kama sehemu ya hati tambulishi zako kwenye huduma ya akaunti ya Microsoft wakati unapoingia kwenye tovuti au huduma na akaunti yako ya Microsoft. Huduma ya akaunti ya Microsoft hutuma maelezo yanayofuata kwenye tovuti au huduma ambayo umeingia: Namba ya kitambulishi cha kipekee ambayo huruhusu tovuti au huduma kubainisha kama wewe ni mtu yule yule kutoka kwa kipindi kimoja cha kuingia hadi kingine; namba ya toleo iliyopangiwa akaunti yako (namba mpya hupangiwa kila wakati unapobadilisha maelezo yako ya kuingia); iwe anwani yako ya barua pepe imethibitishwa; na iwe akaunti yako imelemazwa.
Tovuti na huduma zingine za wahusika wengine ambazo hukuruhusu kuingia na akaunti yako ya Microsoft uhitaji anwani yako ya barua pepe ili kukupa huduma zao. Katika visa hivyo, wakati unapoingia, Microsoft itakupa anwani ya barua pepe lakini sio nywila yako ya tovuti au huduma. Hata hivyo, kama uliunda hati tambulishi zako na tovuti au huduma, huenda ikawa na ufikiaji wenye kikomo kwa maelezo yanayohusishwa na hati tambulishi zako ili kukusaidia kuweka upya nywila yako au kutoa huduma zingine za auni.
Kama ulipokea akaunti yako kutoka kwa wahusika wengine, kama shule, biashara, mtoa huduma ya tovuti, au msimamizi wa kikoa kilichodhibitiwa, mhusika huyo mwingine huenda akawa na haki ya akaunti yako, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuweka upya nywila yako, kuona matumizi ya akaunti yako au data ya maelezo mafupi, kusoma au kuhifadhi maudhui kwenye akaunti yako, na kusitisha au kughairi akaunti yako. Katika visa hivi, utatumia Makubaliano ya Huduma ya Microsoft na masharti yoyote ya ziada ya matumizi kutoka kwa mhusika huyo mwingine. Kama wewe ni msimamizi wa kikoa kilichodhibitiwa na umewapa watumiaji wako akaunti za Microsoft, unawajibika kwa shughuli zote ambazo hufanyika katika akaunti hizo.
Tafadhali kumbuka kwamba tovuti na huduma ambazo zinakuruhusu kuingia na akaunti yako ya Microsoft zinaweza kutumia au kushiriki anwani yako ya barua pepe au maelezo mengine ya kibinafsi ambayo unayatoa kwao kama ilivyofafanuliwa katika taarifa zao za faragha. Hata hivyo, wanaweza kushiriki namba ya kipekee ya kitambulishi iliyotolewa kwao na huduma ya akaunti ya Microsoft na wahusika wengine tu ili kutimiza huduma au shughuli ambayo huenda umeomba. Tovuti au huduma zote ambazo hutumia akaunti ya Microsoft zinahitajika kuwa na taarifa ya faragha iliyochapishwa, lakini hatudhibiti au kufuatilia desturi za faragha za tovuti hizo, na desturi zao za faragha zitatofautiana. Unapaswa kuhakiki kwa makini taarifa ya faragha ya kila tovuti unayoingia ili ubainishe jinsi kila tovuti au huduma itatumia maelezo inayoyakusanya.
Unaweza kufikia maelezo yako ya kibinafsi kwa kwenda kwenye akaunti. Unaweza kufikia jina lako la mtumiaji ikiwa akaunti yako ya Microsoft sio ya kikoa kilichodhibitiwa. Unaweza kubadilisha nywila yako, kubadilisha anwani ya barua pepe, namba ya simu, na swali na jibu la siri wakati wowote. Unaweza pia kufunga akaunti yako ya Microsoft kwa kuenda kwa akaunti, na kisha "Funga akaunti yako." Ikiwa akaunti yako iko katik kikoa kilichodhibitiwa, kama ilivyofafanuliwa hapo juu, huenda kukawa na mchakato maalum wa kufunga akaunti yako. Tafadhali kumbuka kwamba kama wewe ni mtumiaji wa MSN au Windows Live, ukienda kwa akaunti, huenda ukaelekezwa upya kwa akaunti ya tovuti hizo
Maelezo zaidi kuhusu akaunti ya Microsoft inapatikana katika tovuti ya akaunti ya Microsoft.
Jifunze zaidi kuhusu
Hapa chini utapata taarifa faragha za ziada ambazo zinaweza kuwa au zisomuhimu kwako. Nyingi kati ya desturi hizi zilizofafanuliwa ambazo tunakutaka ujue kuhusu lakini hatudhanii ni muhimu kuangazia kila moja ya taarifa zetu za faragha. Na baadhi ya hii ni kusema ya kawaida (kwa mfano, tutafichua maelezo wakati sheria inairuhusu), lakini mawakili wetu hufanya tuiseme hata hivyo. Tafadhali zingatia kwamba maelezo haya sio ufafanuzi kamili wa desturi zetu - haya ni yote kwa kuongezea zingine, maelezo zaidi maalum yako katika taarifa za faragha za kila bidhaa na huduma ya Microsoft unayotumia.
Kwenye ukuras huu:
Ushirikiano na Ufichuaji wa Taarifa Binafsi
Zaidi na mapokezano yaliyoelezwa kwenye kauli ya usiri ya bidhaa au huduma unazotumia, Microsoft huenda ikapokezana au ikatoa taarifa nafsi:
Huenda pia tukashiriki au kufichua maelezo ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na maudhui ya mawasiliano yako:
Tafadhali kumbuka kuwa tovuti zetu zitajumuisha viungo kwa tovuti za nafsi ya tatu ambazo sera zao za usiri huenda zikawa tofauti na za Microsoft. Ukiwasilisha maelezo ya kibinafsi kwa tovuti zozote hizo, maelezo yako husimamiwa na taarifa za faragha kwenye tovuti hizo. Tunakuhimiza uhakiki kauli za usiri za tovuti yoyote unatembelea.
Kulinda Usalama wa Taarifa Binafsi
Microsoft ni nia ya kulinda usalama wa taarifa zako binafsi. Tunatumia teknolojia na taratibu mbalimbali za usalama ili kusaidia kulinda maelezo yako ya kibinafsi dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa, matumizi, au ufichuzi. Kwa mfano, tunahifadhi maelezo ya kibinafsi tunayotoa kwenye mifumo ya kompyuta yenye ufikiaji wenye kikomo na yako katika katika suhula zilizodhibitiwa. Tunaposambaza taarifa ya usiri mkuu (kama vile nambari ya kadi ya mkopo au nenosiri) kwenye mtandao, tunailinda kupitia matumizi ya usimbaji fiche, kama vile itifaki ya Utepe Salama wa Soketi (SSL).
Kama nenosiri linatumiwa kulinda akaunti ya ko na taarifa binafsi, ni jukumu lako kuweka nenosiri lako siri. Usiyashiriki. Kama unatumia tarakilishi, sharti utoke kabla ya kujitoa tovutini au huduma ili kulinda ufikivu wa taarifa yako kutoka kwa watumiaji wa mara kwa mara.
Ambamo Taarifa Inahifadhiwa na Kuchakatwa.
Taarifa binafsi inayokusanywa kwenye tovuti na huduma za Microsoft zinahifadhiwa na kuchakatwa Marekani au nchi yoyote ambapo Microsoft au washirika wake, matawi au watoaji huduma hutunza nyenzo. Microsoft inatii Mpangilio wa Bandari Salama wa U.S.-EU pamoja naule Mpangilio wa Bandari SalamaU.S.Swizi kama ilivyowekwa wazi na Idara ya Biashara U.S. kuhusiana na ukusanyaji, matumizi na ubakizi wa data kutoka kwenye eneo la Kiuchumi Ulaya, na Uswizi. Ili kujifunza zaidi kuhusu Programu ya Bandari Salama, na kuonyesha udhinishaji wetu, tafadhali tembelea http://www.export.gov/safeharbor/.
Kama sehemu ya kushiriki kwa Microsoft katika programu ya Safe Harbour, tunatumia TRUSTe, mhusiku huru wa kando, katika kuweza kutatua mizozo unayoweza kuwa nayo nasi kuhusiana na sera na shughuli zetu. Kama ungependa kuwasiliana na TRUSTe, tafadhali tembelea https://feedback-form.truste.com/watchdog/request.
Microsoft huenda ikahifadhi taarifa binafsi yako kwa sababu nyingi, kama kuenda sawa na masharti yetu, kusuluhisha mzozo, kutekeleza maagano yetu na zaidi kutoa huduma. Kujifunza ni vipi unafikia taarifa zako za kibinafsi, tembelea Ufikiaji wa Taarifa yako.
Mabadiliko ya Kauli Zetu za Faragha
Tutakuwa kila wakati tukisasisha kauli za usiri kuangazia majibu ya wateja na mabadiliko katika huduma zetu. Tunapoweka mabadiliko katika kauli yetu au ni vipi Microsoft inakavyotumia taarifa yako ya kibinafsi. Ikiwa kuna mabadiliko ya rasilimali kwenye taarifa hii au katika jinsi Microsoft itatumia maelezo yako ya kibinafsi, tutakuarifu aidha kwa kuchapisha notisi mara moja juu ya mabadiliko hayo kabla ya kuyatekeleza au kwa kukutumia taarifa moja kwa moja. Tunakuhimiza uhakiki kauli za usiri kwa bidhaa na huduma unazotumia kusoma ni vipi Microsoft inalinda taarifa yako.
Ni Vipi Unawasiliana Nasi
Microsoft Privacy, Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, Washington 98052 USA
Ili kupata tanzu ya Microsoft katika nchi yako au eneo, tazama http://www.microsoft.com/worldwide/.
Vumbuzi vya Faragha vya FTC
Usalama nyumbani
Trustworthy Computing